Social Icons

Pages

Wednesday, 14 May 2014

GIGGS KIMYAKIMYA ATUA UHOLANZI KUBONGA NA VAN GAAL





Ryan Giggs ametua nchini Uholanzi tayari kukutana na kocha mtarajiwa wa Manchester United, Louis van Gaal.
Giggs atakutana na Van Gaal katika eneo la Noordwijk, karibu kabisa na timu ya taifa ya Uholanzi ilipoweka kambi kujiandaa na Kombe la Dunia.
Giggs mwenye umri wa miaka 40 alionekana kwenye hoteli moja karibu na kambi hiyo leo mchana na ilielezwa alikuwa tayari kukutana na Van Gaal.
Tayari Van Gaal amekubali kutua Man United kuchukua nafasi ya David Moyes na amepewa masharti ya kufanya kazi na Giggs ambaye ndiye mchezaji mkongwe zaidi Man United kwa sasa
 
FULU VIWANJA