Jumapili 13 Aprili 2014
1537 Liverpool v Man City
1807 Swansea v Chelsea
LIVERPOOL v MAN CITY
Hii ni Bigi Mechi na pia muhimu katika
mbio za Ubingwa kwani Liverpool wapo kileleni mwa Ligi Kuu England
wakiwa Pointi 4 mbele ya Manchester City lakini wao wamecheza Mechi 2
zaidi.
LIGI KUU ENGLAND
MSIMAMO-Timu za Juu:
|
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
|
1 |
Liverpool |
33 |
23 |
5 |
5 |
90 |
40 |
50 |
74 |
|
2 |
Chelsea |
33 |
22 |
6 |
5 |
65 |
24 |
41 |
72 |
|
3 |
Manchester City |
31 |
22 |
4 |
5 |
84 |
29 |
55 |
70 |
|
4 |
Arsenal |
33 |
19 |
7 |
7 |
56 |
40 |
16 |
64 |
|
5 |
Everton |
32 |
18 |
9 |
5 |
52 |
31 |
21 |
63 |
|
6 |
Tottenham Hotspur |
33 |
18 |
5 |
10 |
45 |
45 |
0 |
59 |
|
7 |
Manchester United |
33 |
17 |
6 |
10 |
56 |
38 |
18 |
57 |
Liverpool wanaingia kwenye Mechi hii
wakiwa hawajafungwa katika Mechi 14 za Ligi, wameshinda 9 kati ya hizo,
wakati Man City hawajafungwa katika Mechi 10 za Ligi za Ugenini.
Hali za Wachezaji
Meneja
wa Liverpool Brendan Rodgers itabidi aamue kumchezaji yupi acheze
Sentahafu kati ya Mamadou Sakho na Daniel Agger baada ya wote kupona
maumivu yao lakini watamkosa Jose Enrique ambae bado kaumia ila Joe
Allen anaweza kuanza ikiwa Rodgers ataamua anahitaji Kiungo wa ziada
kwenye safu hiyo.
Man City wao wana faraja kubwa baada ya
Mfungaji wao Bora Sergio Aguero, aliekosa Mechi 5, kupona na sasa yuko
fiti kwa Mechi hii.
Lakini City itaendelea kumkosa Matija Nastasic ambae ana tatizo la Goti.