MLINDA
Mlango wa timu ya DR Congo, Robert Kidiaba anaamini jukumu lake jipya katika
timu hiyo kama balozi wa amani, kunaweza kusaidia kuunganisha nchi yake sehemu
mbalimbali duniani.
Golikipa
huyo mwenye umri wa miaka 38, anaamini nchi yake haitakuwa na maendeleo bila kuwepo
na amani.
Kwa
miaka kadhaa, Congo imekuwa kwenye migogoro na kutokea mauaji ya kutisha kutokana
na rasilimali kubwa za asili zilizopo nchini hapo.
“Miaka mingi ya vita imetufanya tuchelewe kupata
maendeleo ya nchi yetu, najua kwamba si rahisi kumshirikisha mtu katika
mchakato wa amani hapa Congo, kwakuwa nchi imekuwa ikikabiliwa na vita,”
alisema Kidiaba.
[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[[
SHIRIKISHO
la Soka nchini hapa FA, limesema timu yake ya Burkina Faso itacheza mechi ya kirafiki na timu ya Morocco,
Mei 24 mwaka huu nchini Ureno.
Mwenyekiti
wa shirikisho hilo, Sita Sangaré amesema kwenye mkutano w maandalizi ya
kushiriki fainli za AFCON zitakazofanyika nchini Morroco mwakani.
Burkina
Faso na Morocco zilishindwa kufuzu kushiriki fainali za kombe la Dunia mwaka
huu, lakini upande huo ulisema kwamba timu yao haikuwa imara kushiriki fainali
za Brazil.
Morocco
bado haijapata kocha wakati ikijiandaa na Uchaguzi wa mwenyekiti wa Shirikisho hilo,
Aprili 13 mwaka huu.
KLABU ya Inter Milan ya nchini ITALI,A
imepanga kurejea nchini Englan kusaka wachezaji nyota, ambapo inamtizamia
kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel.
Rais wa Inter, Erick Thohir alikuwepo
dimba la Stamford Bridge wakati The Blues ilipoizaba mabao 2-0 Paris
Saint-Germain katika robo fainali ya Ligi ya Mabigwa iliyochezea juzi.
Kiungo huyo, amecheza mechi tisa za Ligi
Kuu England chini ya kocha Jose Mourinho tangu aliporejea Chelsea, na ana uwezekano
wa kutimkia Nerazzurri.
Thohir, amekuwa na mahusiano mazuri na
klabu za Ligi England na amepanga kuwaleta wachezaji katika mji wa San Siro,
majira ya joto.
Lassana Diarra
MWANASHERIA wa Kiungo wa Mali, Lassana
Diarra na klaku za Real Madrid, Arsenal na Chelsea, Eric Dupond Moretti, amekanusha
taarifa iliyodai kwamba mteja wake atajihusisha na Uasi nchini Syria.
Vyombo vya habari vya kijamii vilidai
kwamba kiungo huyo wa zamani wa Ufaransa, ambaye anayeichezea klabu ya mjini
hapa, Lokomotiv atakwenda mashariki ya Kati kumpinga rais Bashar Al-Assad.
“Diarra, hawezi kwenda Syria, na hawezi
kuwa muasi bali ataendelea kuchezea mpira wa miguu,”alisema Eric Dupond
Moretti.