Social Icons

Pages

Monday, 10 March 2014

VITI VILIVYOVUNJWA YANGA NA AL AHLY SH MILIONI 15, TFF YASEMA SASA ITAKUFA NA MTU


SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limelaani vikali fujo na uhabirifu wa mali unaofanywa na washabiki viwanjani wakati mechi mbalimbali zikiwemo zile za kimataifa na ligi za hapa nchini.
TFF  imeiomba radhi Serikali kwa uharibifu wa viti uliotokea kwenye mechi ya Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga ya Tanzania na Al Ahly ya Misri iliyochezwa Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Machi 1, mwaka huu.
Imesema uharibifu huo wa viti umesababisha hasara ya Sh. milioni 15 kwa wamiliki wa uwanja huo ambao ni Serikali. TFF tutalipa fedha hizo kwa Serikali kutokana na uharibifu huo.
 Mashabiki wa Timu ya Simba wakiendelea kuwarushia viti Mashabiki wa timu ya Yanga kabla hata ya mtanange wenyewe kuanza uwanjani hapa.
 Viongozi wa timu ya Yanga wakiwaomba Mashabiki wao kuhama katika eneo hilo na kwenda kujibana katika eneo walilotengewa kama wana Yanga. 
“Tunaendelea kuchunguza tukio hilo, huku tukijiandaa kutoa adhabu kwa klabu na washabiki husika kulingana na kanuni zetu. Adhabu itakuwa kali ili iwe fundisho kwa wengine,”imesema taarifa ya TFF.
Kwa mujibu wa Serikali, viti 10 viling’olewa na kutupwa ovyo ovyo uwanjani wakati vingine 40 viliathirika kutokana na vurugu za watazamaji hao na TFF imekubali kubeba dhamana ya kulipa uharibifu huo kwa kuwa wao ndio wenye dhamana ya kusimamia mechi za kimataifa na ndiyo walioomba idhini ya kutumika uwanja huo kwenye mechi hiyo.
“Kwa vile sasa baadhi ya washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu mbalimbali nchini wanataka kufanya suala la uharibifu kuwa la kawaida na mazoea, Serikali inakusudia kuchukua mapato yote ya mchezo husika endapo kutatokea uharibifu,”.
“Pia kuruhusu uwanja kutumiwa bila watazamaji kwa baadhi ya mechi, na kutoruhusu uwanja huo kutotumika kabisa kwa baadhi ya mechi,”imesema taarifa ya TFF.
 
FULU VIWANJA