Social Icons

Pages

Saturday, 15 February 2014

UEFA CHAMPIONZ LIGI: GERARD PIQUE AIONYA MAN CITY!!


BARCA-MESSI_N_NEYMARGerard Pique ameionya Manchester City kwamba tishio toka kwa Barcelona litakuja Uwanja mzima na si toka kwa Lionel Messi tu.
Jumanne Februari 18, Man City wataikaribisha Barcelona Uwanja wa Etihad katika Mechi ya Kwanza ya UCL, UEFA CHAMPIONZ LIGI, ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16.
Pique, ambae aliichezea Man United, Mahasimu wakubwa wa Man City, amesema anangojea kwa hamu pambano hilo na kusisitiza Barca hawamtegemei Messi peke yake kwani wanao Wachezaji wengine ambao ni tishio kama vile Straika wa Brazil, Neymar, pamoja na Pedro na Alexis Sanchez.
Pique ametamka: “Neymar bado mdogo lakini ana kiu kubwa kuionyesha Dunia kwamba yeye ni sahihi kwa Barca na ni mmoja wa Wachezaji Bora Duniani. Kama sio Siku ya Messi, tunae Neymar, tunae Pedro, tunae Alexis, tuna Mastraika wengi hatari.”
Aliongeza: “Kila kitu ilikuwa Messi na kila Mtu alitaka kumzuia yeye. Sasa tuna njia nyingine!”
Ingawa Pique amesema Barca ni tishio lakini vile vile amekiri Man City, chini ya Meneja Manuel Pellegrini, aliewahi kuongoza Klabu za Malaga na Real Madrid huko Spain, ni tishio.
Pia, Pique amekiri Wachezaji wa City kama vile David Silva na Kun Aguero ni hatari.
UEFA CHAMPIONZ LIGI
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA
[Saa za Bongo]
Jumanne Februari 18
22:45 Manchester City v FC Barcelona
22:45 Bayer 04 Leverkusen v Paris Saint-Germain
Jumatano Februari 19
22:45 AC Milan v Atletico de Madrid
22:45 Arsenal FC v Bayern Munich
Jumanne Februari 25
20:00 Zenit St. Petersburg v BV Borussia Dortmund
22:45 Olympiacos CFP v Manchester United
Jumatano Februari 26
22:45 Schalke 04 v Real Madrid CF
22:45 Galatasaray Spor Kulübü v Chelsea FC
MARUDIANO
Jumanne Machi 11
22:45 Bayern Munich v Arsenal FC
22:45 Atletico de Madrid v AC Milan
Jumatano Machi 12
22:45 FC Barcelona v Manchester City
22:45 Paris Saint-Germain v Bayer 04 Leverkusen
Jumanne Machi 18
22:45 Chelsea FC v Galatasaray Spor Kulübü
22:45 Real Madrid CF v Schalke 04
Jumatano Machi 19
22:45 BV Borussia Dortmund v Zenit St. Petersburg
22:45 Manchester United v Olympiacos CFP
 
FULU VIWANJA