MSHAMBULIAJI wa zamani wa klabu ya Yanga SC ya Dar es Salaam, Omar Changa amefariki dunia usiku wa kuamkia Jumapili, Februari 2, mwaka huu kwa ajali ya pikipiki maeneo ya Jangwani, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Moro United, Rodgers Peter klabu aliyokuwa anachezea marehemu Changa mara ya mwisho, mwili wa marehemu uliokotwa maeneo ya Jangwani usiku wa kuamkia Februari 2.
![]() |
Pumzika kwa amani; Omar Changa wa tatu kutoka kushoto waliosimama akiwa na kikosi cha JKT Ruvu |