pucha na salehe ally.
![]() |
| KAZIMOTO KAZINI... |
Kiungo Mtanzania nyota wa Al Markhiya inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza nchini Qatar, Mwinyi
Kazimoto ameweka rekodi ya kucheza mechi 11 zote kwa dakika 90.
Kazimoto
aliyetokea Simba na kujiunga na Al Markhiya, ameweka rekodi hiyo baada ya
kupiga mechi hizo 11, kimahesabu, amepiga dakika 990.
Kutokana na
mwendo huo, Kazimoto ameisaidia timu yake kushinda mechi tatu mfululizo na sasa
iko katika nafasi ya nne ikiwa na pointi 21.
![]() |
| KAZIMOTO AKIWA NA KIKOSI CHA AL MARKHIYA |
Akizungumza
na MOJA YA MTANDAO kutoka Doha, Kazimoto alisema wakati ligi ya nchi hiyo
inaendea ukingoni, ugumu umekuwa ukiongezeka.
“Mechi ya
mwisho pia tumeshinda, tulicheza dhidi ya timu ambayo ni ngumu na inapewa hata
nafasi ya kutwaa ubingwa.
“Kadiri
ligi inavyosonga ukingoni, mambo yanazidi kuwa magumu kwa kuwa ushindani
unaongezeka,” alisema.
Kazimoto ameaminika katika kikosi hicho licha ya kuwa na wachezaji kutoka sehemu mbalimbali duniani, ndiye amepewa dimba la juu, yaani namba nane.

