Klabu ya AS
Cannes inayoshiriki Ligi Daraja la Nne nchini Ufaransa, hatimaye imenyoosha
mikono na kutangaza kumuuza beki wake Shomari Kapombe.
Uongozi wa
AS Cannes umesema bei ya Kapombe ambaye bado yuko hapa nchini ni euro 70,000
(Sh milioni 154) huku ikitaja majina ya klabu mbili, Yanga na Azam FC
wanakaribishwa kuanza mazungumzo.
Awali, tuli pata taarifa za ndani kuhusiana na uamuzi huo, lakini uongozi
ukawa mgumu kulizungumzia.
Lakini
jana
mchana, mmoja wa viongozi wa AS Cannes, Pierre Pilorget alizungumza na alisema wamefikia uamuzi huo na klabu za Tanzania
zilizokuwa zinamtaka
zinaweza kufanya mazungumzo na wakala wake au klabu hiyo.
“Waambie
Yanga kuwa sasa Kapombe tumemuweka sokoni, wanaweza kumpata na bei ndiyo hiyo.
Kama tulivyosema awali wasipite njia za mkato.
“Njia nzuri
ni kufika kwetu na kuzungumza, wakiona hawawezi kufanya hivyo wazungumze na
wakala wake naye atafika kwetu,” alisema Pilorget.
Alipoulizwa
jana kutoka Uholanzi, wakala wake Denis Kadito alisema angependa kuliacha suala
hilo lizungumziwe na klabu.
“Tukianza
kuzungumza wote tutachanganya mambo, nafikiri tuiache klabu ndiyo ilizungumzie
suala hilo,” alisema Kadito.
Simba
ilimpeleka Kapombe AS Cannes bila ya malipo huku ikusubiri kama atauzwa,
itapata asilimia 40 ya mauzo yake.