KIUNGO
Jack Wilshere ameposti picha inayomuonyesha akipigana na mchezaji
mwenzake Mathieu Flamini baada ya mazoezi jana kwenye basi la timu.
Viungo
hao wawili walipigwa picha wakionekana kutofautiana kwenye mazoezi ya
timu hiyo saa 24 kabla ya Arsenal kuwakaribisha Black Cats katika mchezo
wa Ligi Kuu.
Wote utani: Wilshere ameposti picha hii inayomuonyesha akipigana na Mfaransa huyo kwenye basi la timu


Nipishe:
Jack Wilshere amehusishwa na kutofautiana na mchezaji mwenzake Mathieu
Flamini kwenye mazoezi ya Arsenal jana na Bacary Sagna anaonekana kwenda
kusuluhisha

Utaniambia nini: Wilshere akiongea kwa ishara ya mikono na Flamini huku Sagna akimfuata kumtuliza
Bacary Sagna alijitolea kutuliza hasira za wawili hao kwa kumsihi Wilshere atulie.
Lakini
Wilshere akatweet kwa utani baadaye: "Flam hakufurahia wakati naondoka
kwenye basi usiku! Samahani mwenzangu, naahidi kutotofautiana nawe
tena!! #Hasira'
Sakata
la wachezaji hao wawili wa Arsenal linakuja siku kadhaa baada ya
Flamini kutaka kugombana hadharani na Mesut Ozil wakifungwa mabao 2-0 na
Bayern Munich Uwanja wa Emirates
Kiungo huyo Mfaransa alimvaa Ozil akimtuhumu mchezaji huyo aliyenunuliwa kwa Pauni Milioni 42.5 kutojituma kwenye mechi hiyo.
Arsenal
wanarejea uwanjani leo kumenyana na Sunderland katika Ligi Kuu ya
England wakitoka kutoa sare na Manchester United na kufungwa na
Liverpool katika mechi zao mbili zilizopita.