Social Icons

Pages

Friday, 10 January 2014

YAYA TOURE MCHEZAJI BORA AFRIKA KWA MARA YA TATU




Kiungo nyoyta wa Manchester City ya England, Yaya Toure amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mara ya tatu mfululizo.
 
Ushindi huo unamfanya Yaya afikie rekodi ya kushinda mara tatu mfululizo tuzo hiyo, awali mchezaji pekee aliyekuwa ameshinda namna hiyo ni Samuel Eto’o wa Cameroon.

Yaya raia wa Ivory Coast ambaye hivi karibuni alitwaa tuzo ya BBC, amewashinda kiungo wa Chelsea, John Obi Mikel aliyeshika nafasi ya pili na nafasi ya tatu ikaenda kwa Didier Drogba.

Eto’o alishinda tuzo hiyo mara tatu mfululizo baada ya kushinda kuanzia 2003 hadi mwaka 2005. Lakini Mcameroon huyo bado anashikilia rekodi nyingine ya kuwa mchezaji pekee aliyeshinda tuzo hiyo mara nne.
 
FULU VIWANJA