NYOTA
watatu wa Real Madrid wanaounda safu kali ya ushambuliaji iitwayo ‘BBC’
wameifanya timu yao izifikie kwa pointi Barcelona na Atletico Madrid
kileleni mwa Liga kufuatia kufunga mabao katika ushindi wa mabao 5-0
dhidi ya Real Betis inayosuasua mkiani.hapo jana
Nyota hao ‘Bale, Benzema, Cristiano’ umoja wao leo ulikuwa majanga mbele ya kocha wa zamani wa West Brom, Pepe Mel.
Mwanasoka
Bora wa dunia, Ronaldo alifunga bao la kwanza dakika ya 12, Bale
akafunga la pili dakika ya 25, Benzema la tatu dakika ya 45, Di Maria la
nne dakika ya 62 na Morata akahitimisha karamu ya mabao dakika ya 90.
Real
sasa imefikisha pointi 50 za Barca na Atletico, lakini imecheza mechi
moja zaidi, 20 dhidi ya washindani wake hao katika mbio za ubingwa msimu
huu. Barca itakuwa mgeni wa Levante kesho na Atletico Madrid
itaikaribisha Sevilla.
Mbele
kwa mbele: Cristiano Ronaldo ameendelea kusherehekea vyema tuzo ya
Mwanasoka Bora wa Dunia baada ya kufunga bao la kwanza la Real Madrid
katika ushindi wa 5-0 dhidi ya Real Betis
Golazo: Ronaldo alivyofunga leo