Social Icons

Pages

Sunday, 19 January 2014

JUMA NKAMIA NAIBU WAZIRI MPYA WA HABARI ,VIJANA ,UTAMADUNI NA MICHEZO






Kiongozi wa zamani wa Simba, Juma Nkamia ametangazwa kuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo.

Nkamia ambaye ni Mbunge wa Kondoa Kusini (CCM),anachukua nafasi ya Amos Makala ambaye amehamia katika wizara nyingine ya maji.

Nkamia aliyewahi kuwa Katibu Mwenezi wa Simba, ametangazwa leo wakati wa baraza jipya la mawaziri ambalo limetangazwa baada ya baadhi ya mawaziri kufutwa kazi na wengine.
Nkamia ambaye taaluma yake ni mwandishi wa habari amewahi kufanya kazi ya utangazaji katika mashirika mbalimbali likiwemo Redio Tanzania, TBC na yale ya kimataifa kama BBC na Voa.
 
FULU VIWANJA