Social Icons

Pages

Saturday, 18 January 2014

CHAN 2014: CONGO DR YAFUNGWA, BURUNDI USHINDI, MAURITANIA NJE!



CHAN2014_LOGOKundi D la Orange CHAN 2014, Mashindano ya Mataifa ya Afrika kwa Wachezaji wanaocheza ndani ya Nchi zao, limekamilisha Mechi zake za Pili kwa Gabon kuitungua Congo DR Bao 1-0 na Burundi kuicharaza Mauritania Bao 3-2 na kuitupa nje ya Mashindano.
Bao la ushindi kwa Gabon katika Mechi na Congo DR lilifungwa katika Dakika ya Pili tu ya mchezo Mfungaji akiwa Stephane Nguema.
Nayo Burundi ilifungiwa Bao zao za ushindi na Fiston, Nduwarugira na Suleiman Ndikumana ambae pia alikosa Penati huku Bao za Mauritania zikifungwa na Ould Voulany na Taghiyoullah Denna.
Jumapili ni lala salama ya Kundi A ambalo litacheza Mechi zake za mwisho huko Jijini Cape Town kwa Wenyeji South Africa kumaliza na Nigeria, Uwanja wa Cape Town Stadium na Mozambique kuivaa Mali huko Athlone Stadium huku Mechi zote zikianza wakati mmoja.
Ili kusonga, South Africa wanahitaji Sare tu na Nigeria ni ushindi tu ingawa Sare inaweza kuwasaidia ikiwa tu Mozambique, ambayo tayari iko nje ya Mashindano, itaifunga Mali.

MSIMAMO:
KUNDI A
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
South Africa
2
1
1
0
4
2
2
4
2
Mali
2
1
1
0
3
2
1
4
3
Nigeria
2
1
0
1
5
5
0
3
4
Mozambique
2
0
0
2
3
7
-4
0
KUNDI B
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Uganda
2
1
1
0
2
1
1
4
2
Zimbabwe
2
0
2
0
0
0
0
2
2
Morocco
2
0
2
0
1
1
0
2
4
Burkina Faso
2
0
1
1
2
3
-1
1
KUNDI C
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Libya
2
1
1
0
3
1
2
4
2
Ghana
2
1
1
0
2
1
1
4
3
Congo
2
1
0
1
1
1
0
3
4
Ethiopia
2
0
0
2
0
3
-3
0
KUNDI D
NA
TIMU
P
W
D
L
F
A
GD
PTS
1
Burundi
2
1
1
0
3
2
1
4
2
Gabon
2
1
1
0
1
0
1
4
3
Congo DR
2
1
0
1
1
1
0
3
4
Mauritania
2
0
0
2
2
4
-4
0
 
FULU VIWANJA