Kiungo wa Manchester City Yaya Toure
ameungana na Wachezaji wenzake kumtaka Lionel Messi aihame Barcelona na
kujiunga na Timu hiyo ya England.
Awali, Sergio Aguero, ambae anacheza
pamoja na Messi kwenye Timu ya Taifa ya Argentina, aliibuka na kusema
anatamani kucheza pamoja na Messi Klabuni City msimamo ambao Mchezaji
mwingine wa City, Pablo Zabaleta, ambae pia ni Muargentina, aliuunga
mkono.
Lakini Uhamisho wowote ambao utamuhusisha Messi, ambae ndie Mchezaji Bora Duniani, utagharimu Ada ya zaidi ya Pauni Milioni 100.
Hata hivyo, Man City, ambayo inamilikiwa na Matajiri toka Falme za Nchi za Kiarabu, hawawezi kushindwa kulipa Dau hilo.
Uwezekano wa Messi kutua City unaonekana
kuwa kitu kinachowezekana hasa kwa Vile Klabu hiyo hivi sasa inao
Maafisa wa Juu, Ferran Soriano na Txiki Begirstain, ambao walitokea
Barcelona na hivyo kuwa na uhusiano wa karibu na Messi na Kambi yake.
Akiongelea kuhusu Messi, Yaya Toure,
ambae alishawahi kucheza pamoja na Messi wakati akiwa Barcelona,
amesema: “Kama kuja City, natumai Messi atahama Barca.”
Nae Aguero, ambae ni Straika Pacha na
Messi kwenye Timu ya Taifa ya Argentina, amesema: "Ndio, ni bora aje
City. Hakika tutacheza vizuri pamoja. City wamnunue tu."
Lakini Pablo Zabaleta ameenda mbali na
kutoboa kuwa Messi, wakiwa pamoja Kambini na Argentina, huuliza sana
kuhusu maisha huko Etihad.
Zabaleta ametoboa: “Ameniuliza sana kuhusu City. Ni kitu tunachoongelea sana!”
Siku mbili hizi kumeibuka stori kuwa
Messi, ambae kwa Mwezi sasa yuko nje akikabiliwa na maumivu, ana bifu na
uongozi wa Barcelona na hivi Juzi aliibuka na kumponda Makamu wa Rais
wa Barcelona, Javier Faus, kwamba hajui lolote kuhusu Soka baada ya
Kiongozi huyo kupinga kuhusu kufanya majadiliano mapya na Messi kuhusu
Mkataba mwingine mpya.
Hivi karibuni Messi aliongezewa Mkataba na Barcelona hadi Mwaka 2018.
Mwezi Februari, Manchester City itapambana na Barcelona kwenye Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ www,fulu viwanja blogspot.com