Lakini Adebayor, mwenye Miaka 29,
amekasirishwa na kitendo cha Klabu hiyo kutomhusisha kwenye Picha rasmi
ya Wachezaji wa Klabu hiyo na pia kutengwa kufanya Mazoezi na Kikosi cha
Kwanza wakati Meneja akiwa ni Andre Villas-Boas kabla hajatimuliwa Wiki
moja iliyopita.

Adebayor ameeleza: “Ilikuwa ngumu. Nikija Mazoezini naiona Picha ya Timu na mie simo, huko ni kunivunjia heshima.”
Katika Msimu wa 2011/12, Adebayor
alichezea Tottenham kwa Mkopo akitokea Man City na kufunga Bao 17 katika
Mechi 33 na Agosti 2012 alijiunga moja kwa moja na kuwa Mchezaji wa
kudumu wa Tottenham kwa Dau la Pauni Milioni 5.
Katika Msimu uliofuatia wa 2012/13,
Adebayor aliifungia Tottenham Bao 9 tu katika Mechi 36 na Msimu huu
alicheza Dakika 45 tu chini ya Villas-Boas.
Adebayor amesema: “Mie ni Mchezaji wa
Kulipwa, ilibidi nijikaze na kufanya nilichoamriwa. Walitaka nifanye
Mazoezi na Rizevu, nilifanya kwa furaha na walinitaka nifanye Mazoezi
peke yangu, nilifanya kwa furaha.”
Ameongeza: “Sasa kila kitu kinaenda sawa. Nilifanya bidii na sasa naona matunda. Nimefurahi.”
Baada kutimuliwa Villas-Boas, Tim
Sherwood ameshika wadhifa kwa muda kuanzia Wiki iliyopita na mara moja
akamrudisha Adebayor Kundini na katika Mechi ya kwanza tu chini ya
Sherwood, Jumatano iliyopita kwenye Capital One Cup, Adebayor aliifungia
Spurs Bao 1 lakini wakafungwa na West Ham 2-1 na kutolewa nje ya Kombe
hilo.
Katika Mechi iliyofuatia, hapo Jana,
Adebayor alichezeshwa Mechi yake ya Ligi ya kwanza dhidi ya Southampton
na kupiga Bao 2 na Spurs kuifunga Southampton Bao 3-2.www.fulu viwanja blogspot.com