
Erik Lamela pichani juu alikuwa ni mmoja wa wale wanne waliosajiliwa bila ya ridhaa ya Villas-Boas

Nacer Chadli pichani juu pia hakuwa chaguo la Villas-Boas
Andre
Villas-Boas hakuidhinisha usajili wa wachezaji wanne kati ya saba
walikuwa wakitakiwa na klabu hiyo ambapo inadai kuwa alimtaka mwenyekiti
wa klabu Totternham Daniel Levy kutokuwanunua wachezaji hao.
Villas-Boas
alipendelea kuwasajili Erik Lamela, Nacer Chadli, Vlad
Chiriches na Christian Eriksen, ambao waliigharimu Spurs jumla ya pauni milioni £56 maamuzi yake yalitupiliwa mbali.
Meneja
huyo mreno alimtaka mwenyekiti kumnunua Hulk, Joao Moutinho na David
Villa alipokuwa akijipanga na maisha ya kumudu kikosi bila ya Gareth
Bale aliyetimkia Real Madrid.
Hakuna
kati ya hao aliyesajiliwa na kiasi cha pauni milioni £110 kilichotengwa
kilisimamiwa na nguvu nyingine iliyokuwapo White Hart Lane ambayo
ilihitimisha nguvu hiyo kwa kumfuta kazi Villas-Boas Jumatatu iliyopita.
Wachezaji saba pekee ambao walisajiliwa na Tottenham ambao Villas-Boas aliwataka ni Paulinho, Etienne
Capoue na Roberto Soldado. Wengine walitambulishwa na Levy pamoja na mkurugenzi wa ufundi Franco Baldini.
Licha
ya kwamba meneja alipendekeza Levy kuajiri mkurugenzi wa ufundi lakini
mahusiano kati ya Baldini na Villas-Boas hivi karibuni yaliharibika na
Mreno huyo alikabidhiwa wachezaji ambao hakuwapendekeza.

Not a target: Christian Eriksen alifunga magoli 10 akiwa na 's Ajax alisajiliwa akitokea Ajax, na haikuwa ni pendekezo la Villas-Boas.

Vlad news for Andre: Inadhaniwa kuwa Villas-Boas hakumtaka mlinzi wa kimataifa wa Romania Vlad Chiriches

Villas-Boas aliyefutwa kazi baada ya matokeo ya kichapo cha mabao 5-0 Jumapili dhidi ya Liverpool
Villas-Boas
alimtaka Willian kutoka katika klabu ya Anzhi Makhachkala lakini
Tottenham walizidiwa maarifa na Chelsea katika mbio za usajili
wakimsainisha kwa pauni milioni £30 Mbrazil huyo.
Spurs
baadaye alimgeukia Eriksen na kuipatia Ajax pauni milioni £11.5 kwa
Dane, ambaye alianza msimu kwa makeke lakini inaelezwa kuwa mchezaji
huyo hakuwa pendekezo la meneja.
Maumivu makubwa yalitokezea kwa Villas-Boas, kufuatia mapendekezo yake
mengi yahakuweza kusajiliwa.
Hulk
alichomoa kuachana na Zenit St Petersburg na kujiunga na Villas-Boas,
ambaye alifanya naye kazi wakati wakiwa Porto. Pia Moutinho alikuwa
tayari kuelekea kwa bosi wake wa zamani wakiwa Porto licha ya kwamba
mpango wa awali wa kuelekea Spurs uliharibiaka Agosti
2012, ambao ulimchukiza sana Villas-Boas.

Villas-Boas alimtaka Hulk wa Zenit kujiunga naye kiangazi.

Villas-Boas pia alitaka kuungana tena na Joao Moutinho kwasasa akiwa Monaco, ambaye alimfundisha akiwa Porto.
Kiungo
huyo aliondoka Porto kiangazi iliyopita na kujiunga na Monaco sambamba
na James Rodriguez mpango wa pamoja uligharimu pauni milioni £60.
Hulk
na Moutinho walielezewa kuwa pengine wangekuwa ghali lakini Villa
mwishowe aliihama Barcelona na kujiunga na Atletico Madrid kwa ada ndogo
sana ya uhamisho ya pauni milioni £2 na kufunga magoli sita katika
michezo saba ya mwisho hivi karibuni ya La
Liga.
Kati
ya wale ambao hakuwataka imebainika kuwa Lamela amedhihiri kuwa ni
tatizo kubwa kwa klabu hiyo kwasababu alisajiliwa kwa gharama ya rekodi
ya usajili ya klabu kisia cha pauni milioni £30 akitumia mguu wa
kushoto(left-footed winger) akijiunga kama mbadala wa Bale.

David Villa aliigharimu Atletico Madrid kiasi cha pauni milioni £2 alitokea Barcelona. Pia alikuwa akitakiwa na Villas-Boas
Lamela amecheza michezo miwili ya ligi chini ya Villas-Boas, huku michezo minne akitokea benchi na mpaka bado hajafunga goli.
Eriksen
na Chadli hawajafunga katika Premier League wakiaanza michezo mitano na
kucheza kwa ujumla michezo sita kila mmoja huku Chiriches akianza
michezo sita ya ligi na kufunga goli katika mchezo mmoja tu dhidi ya
Fulham.