Mshambuliaji wa Monaco Radamel Falcao anaamini kwamba mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri kuliko staa wa klabu ya Barcelona Lionel Messi.
Mchezaji huyo wa Colombia anawakubali wachezaji wote wawili, ingawa Falcao anaamini Cristiano ni bora zaidi ya Messi.
"Messi
na Cristiano ni wachezaji muhimu na wakubwa duniani leo hii lakini,
kwangu mimi naamini Ronaldo ni bora zaidi," alisema mchezaji huyo mwenye
miaka 27 alipoongea na El Tiempo.
Falcao pia amesema ni
Cristiano Ronaldo anayestahili kuwa mchezaji bora wa dunia katika tuzo
za Ballon D'or zitakazotolewa mwezi ujao ambapo Ronaldo anapambana na
Ribery pamoja na Messi.
