Pigo kwa Manchester United, Andre Iniesta aongeza mkataba Barcelona
Kiungo
wa Barcelona Andres Iniesta ameingia mkataba wa nyongeza na kigogo cha
Hispania Barcelona kwa kusaini miaka miattu mingine ya ziada.
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 29 sasa atasalia ndani ya klabu hiyo mpaka 2018.
Mkataba
wake wa sasa unatarajiwa kumalizika katika kipindi cha miezi 18 ijayo
ambapo taarifa zilikuwa zikiarifu kuwa Manchester United ilikuwa ni moja
ya klabu iliyokuwa ikinyemelea kandarasi yake mwezi Januari au wakati
wa majira ya kiangazi kwa lengo la kuimarisha sehemu yake ya kiungo.
Rais wa Barca andro Rosell amethibtisha kuwa mchezaji huyo atasalia Nou Camp mpaka June 2018.
Iniesta
ameichezea
Barca jumla ya michezo 479 baada ya kujiunga nayo akitokea Albacete
akiwa na umri wa miaka 12 mwaka 1996. Ameshinda ligi ya vilabu bingwa
Ulaya mara tatu na La Liga mara sita.

Iniesta aliisaidia Hispania kutwa kombe la dunia 2010 .
Kiungo
huyo wa Hispania ameifungia Barca magoli 48 na kuwa msaada katika
kikosi tangu alipoaanza kucheza kama mchezaji wa kutumainiwa October
2002, ameisaida Brca kushinda jumla ya mataji 16 katika kipindi cha
miaka mitano na nusu iliyopita
Sherehe za usajili wake zitafanyika Jumatatu Nou Camp.