Social Icons

Pages

Monday, 30 December 2013

MESSI DIMBANI JANUARI 5 NOU CAMP!!


MESSI DIMBANI JANUARI 5 NOU CAMP!!
LIONEL_MESSI-HUZUNIJAVIER ALEJANDRO MASCHERANO amefurahishwa na habari njema kwamba yule Mchezaji Bora Duniani wanaetoka Nchi moja Argentina na kucheza Klabu moja FC Barcelona ya Spain, Lionel Messi, sasa anaelekea kuwa fiti kabisa baada kuwa nje ya Uwanja akijiuguza maumivu ya Musuli za Pajani [Hamstring].
Mesii aliumia Novemba 11 wakati wa Mechi ya La Liga ambayo Barcelona waliitwanga Real Betis Bao 4-1.
Hivi sasa La Liga iko Mapumzikoni na itarejea tena Januari 4 na Messi anatarajiwa kuichezea Barcelona hapo Januari 5 watakapocheza Uwanja wa Nyumbani Nou Camp dhidi ya Elche CF.
Mascherano amepasua: “Nilikuwa nikiongea na Leo wakati yu mgonjwa. Sasa najua yuko fiti na amepona kabisa!”
Wakati Messi hayupo Kikosini Barcelona, Timu hiyo ilifanikiwa kufuzu kutinga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UEFA CHAMPIONZ LIGI lakini kwenye La Liga ule uongozi wao wa Pointi kadhaa juu kileleni ulikatwa na Atletico Madrid ambao sasa wamefungana kwa Pointi kileleni wakiwa na Pointi 46 kila mmoja baada ya Mechi 17 na Real Madrid wako Nafasi ya Tatu wakiwa na Pointi 41.
LA LIGA
MSIMAMO:
[Kila Timu imecheza Mechi 17]
1 Barcelona Pointi 46
2 Atletico Madrid 46
3 Real Madrid 41
4 Athletic Bilbao 33
5 Sociedad 29
6 Villarreal 28
7 Sevilla 26
8 Getafe 23
9 Espanyol 22
10 Malaga 20
11 Valencia 20
12 Granada 20
13 Levante 20
14 Elche 17
15 Celta Vigo 16
16 Almeria 16
17 Valladolid 15
18 Osasuna 15
19 R Vallecano 13
20 Real Betis 10
 
FULU VIWANJA