Romelu Lukaku amesisitiza kuwa hana matatizo yeyote na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho.
Lukaku, mwenye Miaka 20, ambae yupo kwa
Mkopo Everton tangu mwanzoni mwa Msimu huu akitokea Chelsea, amekanusha
habari zili
zozagaa kuwa kutuwa kwake huko Goodison Park ni kutokana na
bifu na Mourinho.
Akiwa na Everton, Lukaku, ambae pia huchezea Timu ya Taifa ya Belgium, amefunga Bao 8 katika Mechi 13.
Lukaku ameeleza kuhamia kwake kwa Mkopo
huko Everton ni matakwa yake yeye mwenyewe ili apate nafasi ya kucheza
mara kwa mara ili ajiendeleze zaidi baada ya Msimu uliopita pia kucheza
kwa Mkopo huko West Brom.
Akiongea na Jarida la Sport Voetbal,
Lukaku alieleza: “Mwanzoni nilisema nataka kubaki Chelsea. Lakini baadae
niliona bora niondoke ili nipate nafasi zaidi ya kucheza. Ni lengo
langu kufanya vizuri zaidi kupita Msimu uliopita. Nataka ni we mmoja wa
Mastraika bora Duniani. Natumai naweza kuwekwa sawa na Cavani,
Ibrahimovic, Van Persie, Suarez na Lewandowski katika Miaka miwili
ijayo.”
Aliongeza: “Nimekuwa na Jose Mourinho
kwa Miezi miwili. Hatukuwa na tatizo. Yeye allitaka nibaki na aliniuliza
kwanini nataka kuondoka!”
Pia Lukaku alihakikisha kuwa atarudi tena Chelsea na ndio maana alisaini Mkataba wa Miaka mitanowww.fulu viwanja blogsop .com