Social Icons

Pages

Friday, 20 December 2013

KOCHA WA SIMBA AMEWAMBIA MASHABIKI WA SIMBA WATULIE ANAJUA DAWA YA OKWI

ocha Mkuu wa Simba, Zdravko Logarusic amewashusha presha mashabiki wa timu hiyo kuhusu makali ya mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye ametua Yanga kwa kusema kuwa dawa yake ipo.

Logarusic ‘Loga’, amesema anatambua kuwa Okwi raia wa Uganda ni mmoja wa washambuliaji bora katika Ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, lakini kamwe hawezi kupata wasiwasi dhidi yake kwa kuwa mabeki wake wanajua kazi wanayotakiwa kuifanya.
Tambo za Loga zinatokana na Simba kumsajili beki wa kati, Donald Musoti kutoka Gor Mahia ya Kenya, huku Joseph Owino na Gilbert Kaze nao wakiwa fiti.
“Nimesikia kuwa kuna kelele nyingi kuhusu Okwi, namjua huyo mchezaji ni mmoja wa wachezaji wazuri ambao nimewahi kuwaona ukanda huu, lakini sidhani kama naweza kupata wasiwasi kwa kujiunga kwake Yanga,” alisema Loga na kuongeza:
“Nimekuwa nikiwafanyia tathmini mabeki wangu, nadhani wanaweza kutusaidia, tumeanza kazi ya kutengeneza safu makini ya ulinzi, tukikamilisha hili haraka, nafikiri inaweza kuwa safu nzuri itakayoweza kupambana na washambuliaji wakali, akiwemo huyo Okwi.”
 
FULU VIWANJA