Timu ya ya Kagera Sugar inatarajia kucheza
mechi nne za kirafiki na timu za Sports Club Villa, Express, URA na Bunamwaya
kutoka Uganda ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu
Bara unaotarajiwa kuanza Januari, mwakani.
Kocha Msaidizi wa Kagera, Mrage
Kabange amesema wameamua kucheza mechi za kirafiki na timu za Uganda kutokana
na ubora wao, pia urahisi wa kuzifikia timu hizo.
“Tunaamini timu hizo zitakuwa kipimo
kizuri kwetu kabla ya ligi kuu, utaratibu wa kucheza na timu hizo utaanza baada
ya wiki mbili kutoka sasa.
