KIUNGO wa Arsenal
Jack Wilshere amekiri Shitaka la Utovu wa Nidhamu toka kwa FA, Chama
cha Soka England, baada kunaswa akitoa ishara ya Kidole kimoja ambayo
huchukuliwa kama matusi wakati Arsenal inapigwa Bao 6-3 na Manchester
City Jumamosi Uwanjani Etihad lakini amepinga Adhabu ya Kufungiwa Mechi 2
ambayo moja kwa moja huambatana na kosa la aina hiyo.
Tukio hilo ambalo lilitokea katika
Dakika ya 67 halikuonwa na Refa Martin Atkinson lakini FA, chini ya
taratibu zake mpya za Msimu huu, Jopo la Marefa Watatu wa zamani
wamelipitia na kuamua lingestahili Kadi Nyekundu kama Refa angeliliona.
Kesi ya Wilshere itasikizwa na Kamisheni ya Nidhamu ya FA hii leo.

MECHI ZIJAZO ZA ARSENAL:
23 Decemba Chelsea (Emirates)
26 Decemba West Ham (Upton Park)
29 Decemba Newcastle (St James Park)
1 Januari Cardiff City (Emirates)
Ikiwa Kamisheni hiyo itamwona na hatia
basi atazikosa Mechi za Arsenal hapo Desemba 23 dhidi ya Chelsea
Uwanjani Emirates na ile ya Desemba 26 huko Upton Park na West Ham.
Hapo Desemba 2011, Luis Suarez
alifungiwa Mechi moja na kupigwa Faini £20,000 baada ya kuwaonyeshea
ishara kama hii ya Wilshere Mashabiki wa Fulham.www.fulu viwanja blogspot.com