MWENYEKITI
wa Kamati ya Usajili ya klabu ya Simba SC ya Dar es Salaam, Zacharia
Hans Poppe amesema kwamba watani wao wa jadi, Yanga SC wameingia mkenge
kumsajili Emmanuel Okwi na labda watamtumia kwenye mchezo wa Nani Mtani
Jembe pekee, lakini zaidi ya hapo hatacheza Jangwani kwenye michuano
yoyote rasmi.
, Kapteni huyo wa zamani wa Jeshi la Wananchi
Tanzania (JWTZ), amesema kwamba Okwi ni mchezaji halali wa Etoile du
Sahel ya Tunisia na hawezi kucheza Yanga.
Okwi
akisaini Yanga SC mbele ya Mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya klabu
hiyo, Mussa Katabaro kushoto na wakili wa mchezaji huyo kulia
“Mimi
sina wasiwasi, naangalia tu sarakasi zao nikiwa najua wataangukia wapi.
Yule mchezaji Yanga wameingizwa mkenge na FUFA (Shirikisho la Soka
Uganda). Kwa sababu, Etoile ilimtoa kwa mkopo SC Villa na ndiyo maana
hata FUFA walipotaka kumtumia katika CHAN, wakaambiwa haiwezekani kwa
kuwa yule ni mchezaji wa Etoile,”alisema Hans Poppe.
Jumapili
Yanga SC ya Dar es Salaam ilitangaza kumsajili mshambuliaji wa zamani
wa Simba SC, Emmanuel Arnold Okwi raia wa Uganda kwa Mkataba wa misimu
miwili na nusu.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Mashindano ya klabu ya Yanga, Abdallah Ahmed Bin Kleb
alisema siku hiyo Dar es Salaam kwamba wamemsajili Okwi na ataanza
kuichezea timu hiyo mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na michuano ya
Afrika.
Etoile
du Sahel ya Tunisia ilimnunua Okwi kutoka Simba SC Januari mwaka huu
kwa dola za Kimarekani 300,000, lakini mchezaji huyo akaamua kuachana na
klabu hiyo na kurejea kupumzika kwao Uganda, kwa madai hakulipwa
mishahara kwa miezi mitatu.
Wakati
huo huo, Etoile hadi sasa haijailipa Simba SC fedha zake za kumnunua
mchezaji huyo na sakata lake limefikishwa Shirikisho la Soka la
Kimataifa (FIFA).
Baada
ya Okwi kukaa bila kucheza kwa miezi sita, Shirikisho la Soka la Uganda
(FUFA) lilimpigania aruhusiwe kurejea nyumbani kuichezea SC Villa ya
huko ili kunusuru kiwango chake.
Hata
hivyo, baada ya kung’ara na timu ya taifa ya Uganda ‘The Ceanes’ nchini
Kenya kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati, CECAFA
Challenge mwezi huu, Okwi amesajiliwa Yanga SC.
Bin
Kleb alisema kwamba walimsajili Okwi tarkiban siku sita zilizopita,
lakini Hati yake ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) ilipatikana Jumapili na
ndiyo maana wakaamua kumtangaza.
Alipoulizwa
kuhusu utata wa sakata lake ambalo limefika hadi FIFA, Kleb alisema;
“Tumefuatilia kote, hadi kwa wanasheria, na tumefanikiwa kupata hadi ITC
yake, nawaambia mashabiki wa Yanga wajue viongozi wao wanafanya kazi,
hatuna stori nyingi, sisi tunafanya vitendo, tunafanya kazi kwa siri
sana,”.
“Na
tumepitia sehemu zote, tumeona kabisa tuko sahihi katika kumsajili
mchezaji huyu na hakutakuwa na tatizo lolote upande wetu,”alisema.