MABINGWA
wa Ulaya, Bayern Munich, Usiku wa jana huko Stade Adrar, Agadir, Nchini
Morocco wameitandika Guangzhou Evergrande FC Bao 3-0 kwenye Mechi ya
Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Dunia kwa Klabu.
Hadi Haftaimu, Bayern Munich walikuwa
mbele kwa Bao 2-0 kwa Bao za Franck Ribery, Dakika ya 40 na Marijo
Mandzukic, Dakika ya 44.
Kipindi cha Pili, kwenye Dakika ya 47,
Mario Goetze aliipa Bayern Bao la 3 na kutinga Fainali ambayo watakutana
na Mshindi wa Nusu Fainali nyingine kati ya Wenyeji Raja Casablanca na
Atlético Mineiro ya Brazil.
Kabla ya Mechi hiyo itachezwa Mechi ya kusaka Mshindi wa 5 kati ya Al Ahly na Monterrey.