VIDIC, VAN PERSIE KUIKOSA LEVERKUSEN!
>>MSIMU HUU BAYARENA: LEVERKUSEN WAMESHINDA ZOTE KASORO SARE NA BAYERN!!
NAHODHA Nemanja Vidic na Robin van
Persie wataikosa Mechi ya Manchester United huko BayArena dhidi ya Bayer
Leverkusen ya Kundi A la UCL, UEFA CHAMIONZ LIGI.
Meneja David Moyes amethibitisha
kukosekana kwao na wote hawakuwemo kwenye Kikosi kilichosafiri leo
kutoka Jiji la Manchester kwenda huko Germany.
Licha ya Vidic kufanya Mazoezi Asubuhi
hii, Moyes amesema: “Wote bado wana maumivu. Wote si maumivu ya muda
mrefu lakini hawapo tayari kwa sasa.”
MSIMAMO:
KUNDI A |
|||||||||
NA |
TIMU |
P |
W |
D |
L |
F |
A |
GD |
PTS |
1 |
Manchester United |
4 |
2 |
2 |
0 |
6 |
3 |
3 |
8 |
2 |
Bayer 04 Leverkusen |
4 |
2 |
1 |
1 |
8 |
5 |
3 |
7 |
3 |
FC Shakhtar Donetsk |
4 |
1 |
2 |
1 |
3 |
5 |
-2 |
5 |
4 |
Real Sociedad |
4 |
0 |
1 |
3 |
1 |
5 |
-4 |
1 |

Hii ni Mechi ngumu kwenye Kundi A ambayo
Mshindi wake ndie atakaefuzu kusonga Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ingawa
kwa Man United hata Sare kwao si mbaya.
Wakiwa kwao BayArena Msimu huu, Bayer
Leverkusen wameshinda Mechi zao zote kasoro moja dhidi ya Mabingwa wa
Germany na Ulaya, Bayern Munich, ambayo walitoka Sare.