Cristiano Ronaldo Jana alifunga Bao
katika Dakika ya 82 na kuwapa Portugal ushindi wa Bao 1-0 walipocheza na
Sweden katika Mechi ya kwanza ya Mchujo ya kusaka Timu 4 za mwisho za
Ulaya kwenda huko Brazil Mwakani kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Bao hilo lilifungwa katika Dakika ya 82 kwa kichwa cha chini ya Ronaldo alipounganisha krosi ya Miguel Veloso.
Sweden, waliokuwa wakicheza kitimu
walipatia nafasi kadhaa kupitia Johan Elmander, Sebastian Larsson na Kim
Kallstrom huku Nyota wao mkubwa Zlatan Ibrahimovic akishindwa kupiga
hata shuti Golini akiwa ndani ya Boksi.
UKRAINE 2 FRANCE 0
Bao za Roman Zozulya, Dakika ya 61, na
Andriy Yarmolenko, Penati Dakika ya 83, zimewapa ushindi Ukraine wa Bao
2-0 walipocheza na France huko Kiev hapo Jana.
Hili ni pigo kubwa kwa France ambao sasa wako hatarini kuzikosa Fainali za Kombe la Dunia kwa mara ya kwanza katika Miaka 20
Katika Dakika za Majeruhi Beki wa France Laurent Koscielny na Oleksandr Kucher walitolewa kwa Kadi Nyekundu.