] Washindi 5 ndio watacheza Fainali za Kombe la Dunia
Ethiopia
wanasafiri kwenda Nigeria kujaribu kupindua kipigo cha Bao 2-1
walichopewa huko kwao Addis Ababa na Mabingwa wa Afrika Nigeria Mwezi
Oktoba na leo wapo Mjini Calabar kujaribu kutimiza hilo na kupata Tiketi
ya kwenda Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia.
Mechi nyingine ya leo itachezwa huko
Casablanca, Morocco kati ya ‘Wenyeji’ Senegal ambao nao wanasaka
kupindua kichapo cha 3-1 walichopewa na Ivory Coast katika Mechi ya
kwanza.
Senegal wanalazimika kucheza nje ya Nchi yao Mechi zao za Nyumbani baada ya kufungiwa kutokana na vurugu Uwanjani.
Ethiopia, chini ya Kocha Sewinet Bishaw,
imemrudisha Kikosini Straika wao Getaneh Kebede anaecheza huko Afrika
Kusini baada ya kuikosa Mechi ya kwanza na Nigeria kufuatia kuumia Goti.
Bosi wa Nigeria, Stephen Keshi, amemwita
kundini Beki Kenneth Omeruo pamoja na Kipa anaedakia Nchini Ufaransa
Vincent Enyeama huku Rueben Gabriel, Chigozie Agbim, Francis Benjamin,
Solomon Kwambe, Azubuike Egwuekwe na Sunday Mba wakiendelea kubaki
kwenye Timu.
Akielezea Mechi ya leo, Stephen Keshi, amesema: “Gemu ya leo na Ethiopia ni muhimu kwa Nchi na Wachezaji wote wanajua hilo!”
Ivory Coast, chini ya Kocha Sabri
Lamouchi, wanahitaji kulinda ushindi wao wa Bao 3-1 dhidi ya Senegal ili
waende Brazil, lakini tayari wana upungufu kwenye Kikosi chao.
Kwenye Mechi hii na Senegal, Ivory Coast
itawakosa Boka Arthur wa VfB Stuffgart, Siaka Tiene wa Montpellier,
ambao ni Majeruhi, pamoja na Cheick Tiote wa Newcastle ambae yupo
Kifungoni baada ya Kadi.
Senegal, ambao wamelazimika kuchezea
Mechi zao za Nyumbani Nchini Morocco baada ya Mashabiki wao kuleta fujo
Uwanjani Mwezi Oktoba 2012 walipocheza Mechi ya AFCON na Ivory Coast
Mjini Dakar, wameendelea kumpiga chini Straika wa Chelsea Demba Ba na
pia kumuacha Beki wa Marseille Souleymane Diawara.
Lakini miamba wengine, kama vile Zarko Toure, Mame Birame Diouf na Pape Kouly Diop, bado wapo kwenye Timu.
TIMU AMBAZO ZIMESHAFUZU
[Jumla 21 Bado 11]:
Europe [Nchi 9 Bado 4]: Belgium, Bosnia-Herzegovina, England, Germany, Italy, Netherlands, Russia, Spain, Switzerland
South America [Nchi 5, Uruguay wapo kwenye Nchujo]: Argentina, Brazil (Wenyeji), Chile, Colombia, Ecuador
Asia [Nchi 4, Jordan wapo kwenye Mchujo]: Australia, Iran, Japan, South Korea
North & Central America/Caribbean [Nchi 3, Mexico wapo kwenye Mchujo]: Costa Rica, Honduras, USA