Kocha
wa kikosi cha timu ya taifa ya Nigeria Stephen Keshi amesisitiza kuwa
haogopi kufukuzwa kazi kabla ya fainali ya kombe la dunia 2014 nchini
Brazil.
Chini ya Keshi Nigeria imefanikiwa kupata tiketi ya kucheza kombe la
dunia baada ya ushindi wa jumla wa mabao 4-1 dhidi ya Ethiopia mchezo
wa hatua ya mwisho ya mtoano.
Mara mbili nahodha huyo wa zamani wa Super Eagles amekuwa akizikosa fainali baada ya kampeni ya mafanikio ya kufuzu.
Mwaka 2002 Keshi alikuwa msaidizi wa Shuaibu Amodu wakati Nigeria
ilipofuzu kombe la dunia lakini wawili hao walifukuzwa kazi na nafasi
zao kuchukuliwa na Adegboye Onigbinde kabla ya fainali kupigwa Korea
Kusini na Japan.
Miaka minne baadaye Keshi alikutana na kadhia kama hiyo ya kufukuzwa
kuelekea kwenye fainali ya mwaka 2006 nchini Ujerumani licha ya
kuongoza kikosi mpaka kufikia fainali kwa mara ya kwanza na sasa
inatazamwa kama wakati wa kurejesha kumbukumbu nyuma.
Amenukuliwa Keshi akisema
“Sihitaji msaidizi kutoka nje kuifanya Super Eagles ifanye vema kombe la dunia”
"kazi hii ni ya kuajiriwa na kufukuzwa "
"nilipokfukuzwa
mwaka 2002 ilikuwa kwangu mshituko lakini haya ni maisha, sawa yote
yamepita kwani huwezi kuendelea kuishi na hasira na kukata tamaa.
"Tunazungumzia juu ya Nigeria hapa, hivyo huwezi juu nini kitatokea.
"lakini kilichomuhimu kwasasa ni kwamba tunaangalia zaidi
kilichombele ambacho ni kuandaa wachezaji wangu na si kitu kingine.