RAIS MPYA WA TFF.JAMALI MALINZI APANGA MIKAKATI YA SOKA LA WANAWAKE
Rais mpya wa Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF), Jamal Malinzi amesema kati ya mambo atakayoanza nayo ni soka la
wanawake.
Malinzi amesema katika mipango ya muda
mfupi atakayoanza nayo ni soka la wanawake.
“Tutahakikisha timu ya wanawake chini ya
miaka 20 inasonga mbele na baada ya hapo, tutaendelea na maandalizi mengine.
“Hakuna namna, lazima tuwaunga mkono kwa
wakati huu kwa kuwa wao ndiyo wako vitani na wanaliwakilisha taifa.
“Suala hilo nitaanza nalo katika mipango
ya muda mfupi, lakini baada ya hapo itakuwa ni mipango ya muda mrefu ambayo
inajumuisha mambo mengi kama kusaka vipaji, vifaa, soka mashuleni na mambo
mengine mengi,” alisema Malinzi.
Timu
ya taifa ya Wanawake chini ya miaka 20, Tanzania iliitungua Msumbiji
kwa mabao 10-0 katika mechi ya kwanza kuwania kucheza Kombe la Dunia
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar na sasa ni maandalizi kwa
ajili ya marudiano mjini Maputo.
Malinzi amechukua nafasi hiyo iliyokuwa
inashikiliwa na Leodeger Tenga baada ya kumshinda Athumani Nyamlani.
Tayari Tenga amesema atamkabidhi Malizi ofisi rasmi keshokutwa saa tano asubuhi.