Mchezaji
mkongwe wa AC Milan Filoppo Inzaghi amedai kuwa rekodi yake ya kufunga
mabao katika michezo ya fainali ya michuano haikuwaja kufikiwa na mtu
yoyote duniani hata awe Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji
huyo ambaye kwasasa ana umri wa miaka 40 alifunga jumla ya magoli nane
katika michezo mbalimbali ya fainali wakati wa kipindi chake cha
uchezaji soka ndani ya vilabu vyote vya Juventus na Milan.
Mkongwe
huyo mtaliano anajivunia zaidi mwaka 2007 alifunga magoli mawili katika
mchezo wa fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya dhidi ya Liverpool mjini
Athens, kabla ya kufunga magoli mengine mawili dhidi ya Sevilla na Boca
Juniors katika michuano ya Uefa Super Cup na Fifa World Club Cup.
Inzaghi
anamatumaini kuwa uwezo huo aliokuwa nao uwanjani hautakuja kufikiwa na
mtu yoyote wakiwemo wachezaji wawili wanaofukuzana mara kwa mara katika
kuwania tuzo ya Ballon d'Or.
"Kocha wetu kipingi kile Carlo
Ancelotti alikuwa hana uhakika wa nani amtumie katika kati yangu na
Alberto Gilardino katika fainali ya Athens, lakini alinipanga mimi na
kufunga magoli yote mawili," alikuwa akiongea na La Gazzetta dello Sport.
"Tena nikafunga katika fainali ya Super Cup dhidi ya Sevilla and na bao lingine dhidi ya Boca Juniors.
"Magoli
matano katika michezo mitatu ya fainali muhimu sana na kushinda michezo
yote hilo ni jambo muhimu sana. Hakuna si Messi wala Ronaldo
atafanikisha hilo.
Ni rekodi nitabaki nayo."