GUS POYET ATAKA KADI NYEKUNDU YA WES BROWN IFUTWE!
>> POYET: “NATAKA CHAMA CHA MAREFA KITUOMBE RADHI!”

Refa wa Mechi hiyo ya Ligi Kuu England,
Kevin Friend, alimtoa nje Wes Brown kwa madai alimchezea faulo Charlie
Adam lakini ukweli ni kuwa Mchezaji huyo wa Stoke City hakuguswa na
Brown aliucheza Mpira tu.
Wiki iliyopita, Mike Riley, Mkuu wa
Marefa, alimpigia Simu Meneja wa West Bromwich Albion, Steve Clarke, na
kumwomba radhi baada ya Refa Andre Marriner kuwapa Chelsea Penati tata
katika Dakika ya 94 na kusawazisha Bao na Mechi kwisha 2-2.
Poyet amesema: “Labda itabidi Mike Riley anipigie Simu. Nitaacha Simu yangu wazi.”
Tukio la kutolewa kwa Wes Brown
lilitokea baada ya Sunderland kufungwa Bao 1-0 Mfungaji akiwa Charlie
Adam na wakati huo Poyet alichukizwa sana na kuwapigia kelele Marefa.
Poyet ameeleza: “Ama tuombwe Msamaha na Kadi ifutwe. Tutakubali kosa la Refa na kusonga mbele!”
Aliongeza: “Ni ngumu kuelewa. Labda Mtu
anieleze kwa maneno mengine. Sidhani kama yapo maelezo! Je ilikuwa rafu
ya Miguu miwili? Hapana. Alikuwa hamiliki Mpira? Hapana. Je alipitisha
Mguu juu ya Mpira? Hapana. Je mpinzani alikuwa hatarini? Hapana.
Alimgusa? Hapana. Tafadhali nieleze. Ni ngumu kukubali!”
Poyet alimalizia: “Nataka Chama cha
Marefa kituombe radhi! Walimpigia Simu Meneja wa Kiingereza na nadhani
sasa ni wakati wa kumpigia Meneja wa Nje!!”