leo ndani ya viunga vya soweto katika dimba la orlando pirates ni mehi ya fainali
MECHI ya kwanza ya Fainali ya Klabu Bingwa Afrika itachezwa huko Afrika Kusini MjiniJohannesburg Uwanja wa Orlando uliopo Kitongoji cha Soweto kati ya Orlando Pirates na Al Ahly ya Egypt.
Timu hizi zitarudiana huko Misri hapo
Novemba 10 na Mshindi ndie atawakilisha Afrika katika Fainali za FIFA za
Klabu Bingwa Duniani zitakazochezwa huko Nchini Morocco Mwezi Desemba.
Msimu huu, Orlando Pirates na Al Ahly,
ambao ndio Mabingwa Watetezi wa Afrika, walikuwa Kundi moja, KUNDI A,
kwenye Mashindano haya ya CAF CHAMPIONZ LIGI na Pirates kushinda Mechi
ya kwanza huko Johannesburg Bao 3-0 na kutoka Sare 1-1.
Lakini, Al Ahly walimaliza wakiwa Washindi wa KUNDI A wakiwa na Pointi 11 na Pirates kuchukua Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 8.