JOSE MOURINHO NAYE AKISEMA HAYA
Jose
Mourinho amesema kiwango kibovu cha timu yake ndiyo sababu ya kupoteza
mchezo wa leo dhidi ya Newcastle na kwamba walistahili kupoteza mchezo
huo.
Blues
waliharibikiwa kabisa kwa magoli ya dakika za majeruhi kutoka kwa Yoan
Gouffran na Loic Remy na kumaliza safari yao ya michezo mitano bila
kupoteza.
Hata hivyo akiongea baada ya mchezo , Mourinho amesema kikosi chake kilistahili nkupoteza mchezo huo.
Chelsea ilipata nafasi nyingi katika kipindi cha kwanza lakini umaliziaji ulikuwa mbovu.