
Afisa huyo amefafanua kuwa zipo Nchi
kadhaa ambazo bado zinasubiriwa kuthibitisha ushiriki wao na pia
udhamini wa Mashindano hayo yatakayochezwa kuanzia Novemba 27 hadi
Desema 12 utaanuliwa rasmi Siku hiyo hiyo ya Ijumaa.
Vile vile, CECAFA imesema kuwa ile
mipango ya awali ya baadhi ya Mechi kuchezwa huko Kisumu na Mombasa sasa
umefutwa na Mechi zote zitachezwa Nairobi ingawa bado upo uwezekano wa
baadhi ya Mechi kuchezwa Miji mingine.
Wakati huo huo, Mabingwa Watetezi wa
Chalenji Cup, Uganda, ambayo ipo chini ya Kocha Milutin ‘Micho’
Sredojevic, imethibitisha kuwa Kikosi chake cha kutetea Taji lake
kitaundwa na Wachezaji wanaocheza Soka lao ndani ya Uganda tu ikiwa ni
Mazoezi yao ya ushiriki wao kwenye Fainali za CHAN zitakazochezwa Mwezi
Januari huko Afrika Kusini, Mashindano ambayo Kanuni yake ni kuchezesha
Wachezaji wale tu wanaocheza ndani ya Nchi zao.
Michuano ya Mwaka huu ya Chalenji Cup
inatarajiwa kushirikisha Nchi zote 12 ambazo ni Wanachama wa CECAFA
pamoja na Waalikwa Zambia na Malawi.
Wanachama
wa CECAFA, Shirikisho la Soka kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati, ni
Wenyeji wa Mashindano haya Kenya, Uganda, Tanzania Bara, Zanzibar,
Rwanda, Sudan, Burundi, South Sudan, Ethiopia, Eritrea, Djibouti na
Somalia.
Mechi za Chalenji Cup Mwaka huu zitarushwa moja kwa moja na Vituo vya TV vya SuperSport, TV ya Taifa ya Uganda na TBC.