
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ambaye alicheza dakika zote za
mchezo wa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Arsenal Jumapili iliyopita tayari
ameshaondolewa katika kikosi cha England kinachojipanga kwa mchezo dhidi
ya Ujerumani na Chile.
Wiki hizo sita zitamuweka Carrick nje mpaka baada ya Christmas, na atakosa michezo sita ya ligi ya England.
Carrick hakuwepo katika mchezo wa ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Fulham Novemba 2 kutokana na matatizo hayo.
Ukiacha mchezo huo mchezaji huyo wa zamani wa Tottenham na West Ham
hajakosa michezo wowote wa mabingwa hao watetezi wa taji la ligi mpaka kufikia sasa.
Carrick atakosa mchezo dhidi ya Spurs Desemba mosi na ataendelea
kuwa nje wakati United watakapo kuwa wakiwafuata West Ham Desemba 21.
United pia watakuwa na michezo dhidi ya Cardiff, Everton, Newcastle
na
Aston Villa kuelekea wiki sita zijazo pamoja na michezo muhimu miwili ya
klabu bingwa Ulaya hatua ya makundi pamoja na mchezo wa robo fainali ya
Capital One dhidi ya Stoke.
Nyota wa kimataifa wa Belgium Marouane Fellaini, aliyejiunga na
klabu hiyo akitokea Everton kwa thamani ya pauni milioni £27.5 mwezi
September, pia atakuwa akifikiriwa kuwemo kikosini.