TOURE AWA BALOZI WA UNEP KATIKA KUOKOA TEMBO
Mchezaji ambaye anamiliki taji la sasa la mwanasoka bora wa mwaka barani
Afrika, Yaya Toure, amechaguliwa kuwa balozi wa Shirika la Kuhifadhi
Mazingira la Umoja wa Mataifa – UNEP
TOUREre amepewa jukumu la kuwa mstari wa mbele katika vita dhidi ya
ujangili na biashara haramu ya pembe za ndovu. Nyota huyo wa klabu ya
Manchester City na timu ya taifa ya Cote d'Ivoire ameonya kuwa uwindaji
haramu wa pembe za ndovu unatishia kuangamiza wanyama hao. Akizungumza
mjini Nairobi baada ya kupewa wadhifa wa kuwa Balozi wa UNEP, Toure
amesema kama hatua haitachukuliwa sasa, huenda mnyama huyo akatoweka
kabisa katika siku za usoni.
Aliongeza kuwa timu ya kandanda ya Cote d'Ivoire inafahamika kama "The Elephants" kama heshima kwa wanyama hao ambao wana nguvu na neema, na ilhali nchini mwake pekee kuna tembo 800 tu waliobaki.
Akizungumza katika makao makuu ya UNEP mjini Nairobi, Kenya, Toure amesema anataka kusaidia kupambana na biashara haramu ya pembe za ndovu ambayo husababisha maelfu ya ndovu kuwindwa na kuuawa kila mwaka.
Ujangili umeongezeka kwa kiasi kikubwa barani Afrika katika miaka ya karibuni na biashara haramu ya pembe za ndovu imeongezeka mara tatu tangu mwaka wa 1998, kwa mujibu wa UNEP.