FERGUSON AWAPA MATUMAINI MAN UNITED.Aliyekuwa kocha wa Manchester United, Sir Alex
Ferguson amesema kuwa wachezaji wa Man U wanaweza kubadili mwanzo wao
mbaya kwenye ligi ya Premier, licha ya kuwa pointi nane nyuma ya timu
inayoongoza ligi hiyo kwa sasa Arsenal.
Ushindi mara mbili wa timu hiyo katika mechi
mbili zilizopita , ina maana kuwa upande wa David Moyes wameweza
kujikomboa kutokana na matokeo mabaya zaidi ya Man U katika mwanzo wa
ligi hiyo, kuwahi kushuhudiwa katika miaka 24 ya klabu hiyo."Man U ndio klabu pekee kuwahi kutoka nyuma kwa pointi na hatimaye kushinda ligi,'' alisema Ferguson
Ferguson, aliyesalia kuwa mmoja wa wakurugenzi wa klabu hiyo , alistaafu kutoka katika wadhifa wa meneja mkuu wa klabu mwishoni mwa msimu baada ya kushinda mataji 38 katika usimamizi wake wa miaka 27.
Naye menaja mpya Moyes anakumwba na wakati mgumu upande wa mashabiki baada ya kuanza vibaya msimu.