Social Icons

Pages

Saturday, 26 October 2013

EL CLASSICO YENYE MAAJABU USIKU HUU .NERMAY AU BALE

Mvuto kwa El Clasico hii ni Klabu zote mbili kuwa na Wachezaji wapya ambao wanaweza kucheza kwa mara ya kwanza kwenye mtanange wa aina hii kwa Barcelona kumchezesha Mchezaji mpya Neymar waliemnunua Msimu huu kutoka Santos ya Brazil na Real kumtumia Gareth Bale alievunja Dau la kununuliwa kwa Bei Ghali Duniani walipomnunua kwa Euro Milioni 100 kutoka Tottenham.
Lakini wakati Neymar akionyesha cheche zake kwenye Timu ya Barcelona, Bale amekuwa akikumbwa na Majeruhi yaliyomfanya acheze Mechi chache tu.

Kocha wa Real, Carlo Ancelotti, amedokeza kuwa Bale ataanza Mechi hii pamoja na Wachezaji wake wapya wengine Isco na Asier Illarramendi huku Cristiano Ronaldo akiongoa majeshi.
Nae, Gerardo Martino, amedokeza kuwa mashambulizi ya Kikosi chake yataongozwa na Lionel Messi na Neymar huku ukiwepo uwezekano wa Beki wao Mkongwe ambae pia ni Nahodha wao, Carles Puyol, kuanza Mechi hii baada ya kurudi tena dimbani akiwa nje akijiuguza Goti lake tangu Mwezi Machi.
MECHI ZA MWISHO:
02-03-2013 Real Madrid: 2 FC Barcelona: 1 [La Liga]
26-02-2013 FC Barcelona: 1 Real Madrid: 3 [Copa Del Rey]
30-01-2013 Real Madrid: 1 FC Barcelona: 1 [Copa Del Rey]
07-10-2012 FC Barcelona: 2 Real Madrid: 2   [La Liga]
29-08-2012 Real Madrid  2  FC Barcelona 1 [Super Cup]
23-08-2012 FC Barcelona 3 Real Madrid 2 [Super Cup]
 
FULU VIWANJA