Social Icons

Pages

Friday, 5 January 2018

RATIBA YAENDELEA KULALAMIKIWA NA VILABU SHIRIKI KUNAKO MICHUANO YA MAPINDUZI CUP

Na Suleiman Ussi  Zanzibar

Vilabu mbali mbali vinavoshiriki michuano ya mapinduzi cup vimekuwa na lawama nyingi kuhusiana na ratiba ya iliopagwa katika mapinduzi cup kwa msimu wa mara hii baada ya lawama hizo kuwa nyingi kipindi hiki kimemtafuta katibu wa kamati hiyo ya mapinduzi cup maalimu khamis Abdallah anaelezea juu ya ratiba hiyo

Image result for MAPINDUZI CUP


Muendelezo wa michuano ya kombe la mapinduzi usiku wa jana umeendelea kupigwa kwa mchezo wake wa tatu kati ya timu ya Simba wakioneshana kazi dhidi ya timu ya Jamuhuri katika mchezo huo timu ya jamuhuri walifungwa bao la mapema kupitia mchezaji John Bocco dk ya 4 timu ya jamuhuri baada ya kufungwa bao la mapema walionesha mchezo mzuri wa kuhakikisha wanarudisha bao hilo lakini hakufanikiwa kupata bao mnamo dk ya 34 timu ya simba waliandikia bao lao la 2  kupitia mchezaji wao Moses kitundu hadi kipindi cha kwanza kinamalizika uwanjani timu ya simba wanaongoza bao 2-0 kuingia kwa kipindi cha pili simba walifanikiwa tena kupata bao la 3 kupitia mchezaji wao Asante Kwasi dk ya 59 huku nao timu ya Jamuhuri walifanikiwa kupata bao 1 la kufutia machozi lililofungwa na mchezaji Mosese Nassoro dk ya 87 hadi firimbi ya mwisho inapulizwa uwanjani timu ya Simba 3 na jamuhuri 1 tumefanikiwa kuzungumza na makocha wa pande zote mbili pamoja na man of the match Mwinyi kazi moto kiupande wa kocha wa timu ya Simba masud Djuma amesema licha ya kupata bao 3 lakini timu yake haikucheza kama alivotaka wachezaji wake walikua wanafanya utani na goli pia amegusia suala la ratiba sio rafiki katika mashindano hayo .

Kiupande wake nae kocha msaidizi wa timu ya jamuhuri mfaume shabani amesema anaenda kujipanga na ligi kuu ya zanzibar kanda ya pemba lakini tayari ameshajifunza mengi kwa timu yake kulingana kiwango waliochonesha kwa timu kubwa walizocheza nazo pia nae amegusia sula la ratiba pia kiupande wake sio rafiki sana ..


Nae man of the match katika mchezo wa jana usiku mwinyi kazi moto amesema amejisikia furaha sana kuchaguliwa mchezaji bora katika mchezo wa jana usiku pia amesema zanzibar kuna vipaji vingi vya soka vinahitaji kuendelezwa ili wafike mbali zaidi ..



Kocha salum baussi ambae pia ni mchezaji wa zamani pia alikua ni mgombea wa uraisi wa chama cha soka zanzibar amesema ujio wa mwenyekiti mpya wa baraza la michezo zanzibar Gullam Abdallah amesema ni mtu wa mpira na muadilifu sana katika michezo lakini zaidi salum baussi anaeleza zaid..


Timu meneja wa club ya Jku mohd kombo ( afandi chimudi ) amewatupilia lawama waamuzi wanaochezesha michuano ya kombe la mapinduzi lawama hizo zimekuja tu mara siku ya jana kupigwa bao 1 -0 katika dk ya mwisho chimudi amesema wanachokifanya waamuzi wa unguja sio haki ..


 
FULU VIWANJA