
Gotze amehangaika sana kupata namba kwenye kikosi cha kwanza cha Pep Guardiola katika klabu ya Bayern Munich
Mchezaji huyo aliyeifungia Ujerumani goli la ushindi Kombe la Dunia amecheza mara 20 tu msimu huu, na amekuwa akikerwa sana kwa kuanzishwa benchi.
Lakini kwa ujio wa Ancelotti Allianz Arena mwisho wa msimu huu, ilionekana kama kiungo huyo atapewa nafasi nyingine kuonyesha uwezo wake.
Hata hivyo chanzo kimoja cha Ujerumani Suddeutsche Zeitung kimedai kuwa Ancelotti amemtaarifu Gotze kwamba ataendelea kuwa mchezaji wa benchi atakapotua kuchukua nafasi ya Guardiola anayetimkia Manchester City mwisho wa msimu.
Habari hii ni kama inamwongezea Gotze kasi ya kwenda Liverpool, klabu ambayo mara nyingi imetajwa kutaka kumsajii mchezaji huyo aliyekulia Borussia Dortmund mikononi mwa Klopp.
Hali kadhalika Goal inatambua kwamba Gotze anatamani kuungana na bosi wa Liverpool Jurgen Klopp.
Klopp anajiamini kwamba anaweza kuipata saini ya Mjerumani mwenzake huyo kwa kiasi cha kati ya paundi milioni 15 na 20, hata hivyo anakumbwa na ushindani kutoka Dortmund ambao wanaitaka saini ya Gotze pia.