Mechi za kuwania kucheza fainali za Mataifa Afrika nchini Gabon mwaka 2017 zimepigwa jana katika hatua ya makundi.
Malawi wakicheza nyumbani dhidi ya Guinea imechapwa bao 3-1, Togo na Tunisia sare 0-0, Rwanda imeichakaza Mauritius 5-0.

Misri imeifunga Nigeria bao 1-0, DR Congo imeicha Angola 2-0, Ethiopia imetoka sare na Algeria 3-3, Liberia imefumua Djibout 5-0.
Na huko Uganda Burkina Faso imelazimisha sare tasa (0-0) Uganda katika mechi iliyochezwa uwanja wa Mandela mjini Kampala.