LIGI KUU England inarejea kwa kishindo Wikiendi hii baada ya kupisha Mechi za Kimataifa na dimba kufunguliwa huko Villa Park kwa Timu ya mkiani Aston Villa iliyomtimua Meneja wao kuwavaa Mabingwa Watetezi Chelsea.

Mechi nyingine za Jumamosi ni Arsenal, wakiwa kwao Emirates, kucheza na Watford, Timu ambayo iliwatoa nishai na kuwatupa nje ya FA CUP hapo hapo Emirates Wiki 2 zilizopita.
Nao City, wenye matumaini hafifu ya Ubingwa huku Nafasi yao ya 4 ikiwa hatarini, wako Ugenini kucheza na Bournemouth.
Dimba la Jumamosi litafungwa huko Anfield kwa mtanange wa kuvutia kati ya Liverpool na Timu ya Pili Tottenham.

Jumapili zipo Mechi 2 na zote ni mvuto mkubwa kwani Vinara wa Ligi Leicester City wako kwao King Power Stadium kucheza na Southampton wakati huko Old Trafford ni Mechi kali kati ya Man United na Everton.
Ratiba
**Saa za Bongo
Jumamosi Aprili 2
1445 Aston Villa v Chelsea
1700 Arsenal v Watford
1700 Bournemouth v Man City
1700 Norwich v Newcastle
1700 Stoke v Swansea
1700 Sunderland v West Brom
1700 West Ham v Crystal Palace
1930 Liverpool v Tottenham
Jumapili Aprili 3
1530 Leicester v Southampton
1800 Man United v Everton