FA, Chama cha Soka England, kinasubiri kupokea Ripoti ya Refa Mike Dean hapo Jumatatu ili kuamua kama watamchukulia hatua Straika wa Chelsea Diego Costa ambae alikuwa chanzo cha vurumai zilizosababisha Beki wa Arsenal Gabriel Paulista kutolewa kwa Kadi Nyekundu.
Costa alikuwa kiini cha mzozo baada ya kumpiga usoni na kisha kumwangusha chini Beki wa Arsenal Laurent Koscielny wakati wa Mechi iliyochezwa Jumamosi huko Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Arsenal 2-0.
Lakini Refa Mike Dean aliamua kuwapa Kadi za Njano wote wawili, Costa na Koscielny, badala ya Kadi Nyekundu kwa Costa kama wengi walivyotarajia.
Mara baada ya tukio hilo ndipo Costa na Paulista wakaanza kuzozana na ndipo Paulista akamfyatua Teke Costa na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Ikiwa Refa Mike Dean atabainisha katika Ripoti yake kuwa aliliona tukio lote la Costa na Koscielny na kuamua ni la Kadi ya Njano basi huenda Costa akanusurika Rungu la FA.
Lakini ikiwa Refa Dean atasema hakuona tukio lote basi ni wazi Adhabu kali itamkabili.
HABARI ZA AWALI:
WENGER ATAKA FA IMCHUNGUZE COSTA!
Chama cha Soka England, kimetakiwa kichunguze kwa nini Straika wa Chelsea Diego Costa ameepuka kupewa Kadi Nyekundu katika Mechi yao ya Ligi Kuu England iliyochezwa Leo Stamford Bridge na Chelsea kuifunga Mtu 9 Arsenal Bao 2-0.
Rai hiyo imetolewa na Meneja wa Arsene Wenger lakini imepingwa vikali na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho aliemtaka Wenger aache kulalamika kila mara.
Katika Mechi hiyo, Sentahafu wa Arsenal Gabriel alitolewa kwa Kadi Nyekundu baada ya kumtia Teke Costa na baadae Kipindi cha Pili Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi za Njano 2 na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.
Wenger amesema: “Huyu Costa atafanya hivi hivi Wiki ijayo na Wiki inayofuata na Siku zote hukwepa Kadi!”
Wenger alieleza: “Siku zote Costa anafanya anachotaka na anabaki Uwanjani lakini wengine wote wakijibu uchokozi wake wanatolewa nje. Alimpiga Koscielny usoni na hakufanywa kitu. Costa ametumia udhaifu wa Refa Mike Dean.”
Lakini Jose Mourinho amejibu tuhuma hizo za Wenger kwa kudai Wenger Siku zote hulalamika tu: “Nimechezea na Wenger mara 15 na mara pekee hakulalamika ni tulipofungwa kwenye Ngao ya jamii.
JARIBU KUTAZAMA MAGOLI YA JANA