Social Icons

Pages

Saturday, 8 August 2015

BAHANUZI, CASLLAS ASAINI WASAINI MKATABA WA MWAKA KILA MMOJA



Straika wa zamani wa Yanga, Said Bahanuzi na aliyekuwa kipa wa Simba, Hussein SharifF ‘Casillas’, wote wamefanikiwa kusaini mkataba wa mwaka mmoja kuichezea Mtibwa Sugar ya Turiani, Morogoro.

Bahanuzi msimu uliopita alikuwa akiitumikia Polisi Moro kwa mkopo akitokea Yanga huku Casillas alikuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiwa na majeraha ya ugoko.

Casillas amesema amesaini mkataba maalum wa mkopo na anaamini ataisaidia timu hiyo kupambana kwenye ligi. Bahanuzi alisema, anashukuru kutua Mtibwa baada ya kuachwa na Yanga na kwani amepewa mkataba rasmi wa mwaka mmoja.


“Nimejiunga na Mtibwa kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kuachana na Yanga, naamini ushirikiano nitakaoupata huku tutaiwezesha timu yetu kufanya vizuri msimu ujao,” alisema Bahanuzi.
 
FULU VIWANJA