Social Icons

Pages

Sunday, 5 April 2015

MAGOLI 25, KADI ZA NJANO 28 NA NYEKUNDU 3 KATIKA LIGI KUU ENGLAND JANA



Ligi kuu ya soka ya England imeingia raundi ya 31 huku michezo 7 ikichezwa katika viwanja tofauti na kushuhudiwa Jumla ya magoli 25 yamefungwa wastani wa magoli zaidi ya matatu kwa kila mechi.

Jumla ya kadi za njano 28 za zilitolewa ikiwa ni wastani wa kadi 4 za njano kwa kila mchezo huku mechi baina ya Man United na Aston Villa na ile ya Everton vs Southampton zikiongoza kwa kutoa kadi chache za njano kadi moja tu kwa kila mchezo.

Jumla ya kdi nyekundu 3 zilitolewa katika mechi zote za jana

Mpambano wa kugombea nafasi 4 za juu unazidi kunoga baada ya Arsenal kupaa mpaka nafasi ya 2 ikiishusha Manchester City baada ya kuilambisha Liverpool bao
4-1 na pengine hiyo inafuta ndoto za Liverpool kuwania nafasi hizo 4.

Manchester United ikiwa nyumbani pia iliivurumusha Aston Villa bao 3-1 na kupanda mpaka nafasi ya 3 katika msimamo wa ligi kuu na kuishusha Manchester City mpaka nafasi ya nne ikiwa ni mara ya kwanza United kuwa juu ya City msimu huu.

WAFUNGAJI WA MAGOLI YA MECHI ZA JANA


☆ Arsenal 4-1 Liverpool

     - Hector Beralin (37')
     - Mesuit Ozil (40')
     - Alexis Sanchez (45')
     - Jordan Henderson (76')p
    - Olivier Giroud (90')

☆ Everton 1-0 Southampton 

     - Phil Jagielka (16')

☆ Leicester City 2-1 West Ham United

   - Estabian Cambiasso (12')
   - Cheikhou Kouyate (32')
    - Andy King (86')

☆ Manchester United 3-1 Aston Villa

   - Ander Herrera (43', 90')
   - Wayne Rooney (79')
   - Christian Benteke (80')
 

☆ Swansea City 3-1 Hull City 

   - Sung-Yeung Ki (18')
   - Bafetimbi Gomis (37',90')
   - Paul McShane (50')

☆ West Brom 1-4 Queens Park Rangers

   - Eduardo Vargas (15')
   - Charlie Austin (37')
   - Bobby Zamora (43')
   - Victor Anichebe (58')
   - Joey Barton (90')

☆ Chelsea 2-1 Stoke City 

    -Eden Hazard (39')
   - Charlie Adam (44')
   - Loic Remy 62

.... Prepared by Edo DC

 
FULU VIWANJA