Social Icons

Pages

Saturday, 4 October 2014

IRAN YAJIZOLEA MEDAL KATIKA MICHUANO YA ASIA


Iran yajizolea medali nyingine 3 za dhahabu Incheon














Wanamichezo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran leo wamefanikiwa kujinyakulia medali tatu za dhahabu katika michezo ya mataifa ya Asia inayofanyika Incheon, Korea Kusini.

Timu ya taifa ya mpira wa wavu ya Iran imeshinda medali ya dhahabu baada ya kuibwaga Japan, bingwa mtetezi, kwenye mechi ya fainali ya michuano ya Asia. 

Timu ya taifa ya Iran imeichapa Japan kwa seti 3-1, kwenye pambano kali la vuta nikuvute. Timu ya mpira ya wavu ya Iran ilikuwa na kila sababu ya kusherehekea ushindi huo, kwani miaka minne iliyopita iliondoshwa na Japan kwenye mechi ya fainali ya mashindano ya Asia huko Guangzhou nchini China. 

Timu ya Iran imepata ushindi huo baada ya kupita miaka 56 bila ya kupata medali ya dhahabu kwenye mchezo wa mpira wa wavu.

Medali nyingine mbili za dhahabu zimepatikana leo kupitia kwa Amir Mehdizadeh katika mchezo wa kareti na Farzan Ashurzadeh katika mchezo wa Taekwondo. Ushindi huo umeiwezesha Iran kujikusanyia jumla ya medali 56, zikiwemo 21 za dhahabu, 18 za fedha na 17 za shaba. 

Iran inashika nafasi ya 5 ikitanguliwa na China, Korea Kusini, Japan na Kazakhstan.

 
FULU VIWANJA