Social Icons

Pages

Saturday, 16 August 2014

SUALA LA BASI LAKE KUKAMATWA KWA DENI, TFF KUCHUNGUZA




Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), limesema litafanya uchunguzi kujua uhakika wa deni unalodaiwa na kampuni ya kutengeneza tiketi ya nchini Kenya.
TFF ilikuwa inadaiwa Sh milioni 140, lakini inaelezwa imelipa Sh milioni 70 na bado basi lake aina ya Youtong linashikiliwa kutokana na deni hilo.
Wambura amesema watafanya uchunguzi, lakini akasisitiza, uchache wa watu wenye baadhi ya mechi kimekuwa chanzo cha deni hilo.
“Unajua kuna wakati mechi zinakuwa na watu wachache sana, lakini wenyewe wame-supply tiketi tu.
“Hivyo ni lazima ulipe na utaona mechi kadhaa zikiwa namna hiyo, deni linaongezeka kwa kuwa mechi hizo zinakuwa hazilipi.
“Kuna mambo ya kuangalia lakini tunaendelea kujitahidi kiasi kilichobakia kimalizike,” alisema Wambura.
Wadau wa soka wameonyesha kushangazwa na taarifa za kukamatwa kwa basi hilo.

fulu viwanja blogspot.com

 
FULU VIWANJA