TP Mazembe ya Jamhuri ya Kodemokrasia ya Kongo (DRC) imeanza vibaya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kufungwa bao 1-0 na El Hilal Omduran usiku huu Uwanja wa Khartoum nchini Sudan.
Katika mchezo huo wa Kundi A, bao lililoizamisha Mazembe lilifungwa na Salah Al Jizoli dakika ya 51 akimalizia pasi ya Bakri Babeker.
Washambuliaji wote wawili wa Tanzania wa TPM walicheza, Mbwana Samatta akianza na Thomas Ulimwengu akitokea benchi dakika ya 66 kwenda kuchukua nafasi ya Rainford Kalaba.
