KOCHA
wa Germany, Joachim Low, amekipunguza Kikosi chake cha Awali cha
Fainali za Kombe la Dunia zitakazochezwa huko Brazil kuanzia Juni 12
hadi Wachezaji 27 na pia kumwingiza Kiungo wa Borussia Monchengladbach
Christoph Kramer.
Wakitarajiwa kuingia Kambini huko Italy Wiki ijayo, Low amewaondoa Wachezaji watatu na kumbadili mmoja.
Beki wa Hamburg, Marcell Jansen,
ametemwa kutoka Kikosi cha Awali cha Wachezaji 30 pamoja na Chipukizi
Leon Goretzka na Max Meyer.
Pia Mchezaji wa Augsburg, Andre Hahn, ametemwa na kubadilishwa na Christoph Kramer.
Akifanya mabadiliko hayo, Low
amefafanua: “Hii haihusu uchezaji Hahn ila tumekuwa na Majeruhi kadhaa
ya Wachezaji wa Viungo na kumwita Kramer kunatupa uwezo wa kubadili Timu
wakati wowote tukiwa Kambini.”
Wachezaji wanaocheza Engalnd, wawili wa Arsenal,
Wachezaji hao 27 watapunguzwa hadi 23 na kuwasilishwa FIFA ifikapo Juni 2.
Huko Brazil, Germany wako KUNDI C pamoja na Ghana, Portugal na USA.
KIKOSI KAMILI:
MAKIPA: Manuel Neuer (Bayern Munich), Roman Weidenfeller (Borussia Dortmund), Ron-Robert Zieler (Hanover 96)
MABEKI: Jerome Boateng
(Bayern Munich), Kevin Grosskreutz (Borussia Dortmund), Erik Durm
(Borussia Dortmund), Benedikt Howedes (Schalke 04), Mats Hummels
(Borussia Dortmund), Per Mertesacker (Arsenal), Shkodran Mustafi
(Sampdoria), Marcel Schmelzer (Borussia Dortmund), Philipp Lahm (Bayern
Munich)
VIUNGO: Lars Bender
(Bayer Leverkusen), Julian Draxler (Schalke 04), Matthias Ginter
(Freiburg), Mario Gotze (Bayern Munich), Christoph Kramer (Borussia
Monchengladbach), Sami Khedira (Real Madrid), Toni Kroos (Bayern
Munich), Thomas Mueller (Bayern Munich), Mesut Ozil (Arsenal), Lukas
Podolski (Arsenal), Marco Reus (Borussia Dortmund), Andre Schurrle
(Chelsea), Bastian Schweinsteiger (Bayern Munich)
MAFOWADI: Miroslav Klose (Lazio), Kevin Volland (Hoffenheim)